Anti-Discrimination Board
spacer
print  Print page  
Swahili: What can I do if I have been discriminated against in New South Wales?

Kuna mtu yeyote aliyewahi kutokukutendea haki au kukubagua?

Baadhi ya aina za ukiukazi wa haki (ubaguzi) ni kinyume cha sheria
Hapa kuna mifano kadhaa inayoelezea hali hiyo:

  • Watu wa kazini kwako wanakucheka kwa sababu ya lafudhi yako.
  • Bosi wako anakufukuza kazi kwa sababu wewe ni mja mzito.
  • Mtu anakataa kukupangisha nyumba kwa sababu ya rangi yako, au kwa sababu una watoto, au kwa sababu hujaoa au koulewa.
  • Kuna mtu kazini kwako ambaye anagusa mwili wako ingawa hutaki afanye hivyo, au kukusemea maneno machafu ya kimapenzi ambayo huyataki.
  • Mwenye duka anakataa kukuhudumia kwa sababu unatoka nchi nyingine
  • Mkubwa wako wa kazi anakufukuza kazi kwa sababu hufiki kazini ili kumuuguza mtoto wako anayeumwa.

Nani wanaweza kukusaidia?
Bodi ya Kuzuia Vitendo vya Ubaguzi pengine inaweza kukusaidia endapo mtu hakutendei haki au kukubangua kwa sababu ya:
  • kabila, rangi, lugha, mavazi ya kidini au lafudhi
  • jinsia (kwa sababu wewe ni mwanamke au mwanamume)
  • uja uzito
  • umri
  • ulemavu (wa mwili, akili, moyo, au kutoweza kujifunza au maradhi)
  • hadhi yako ya ndoa (kwa sababu umeoa/kuolewa, hujaoa/kuolewa, unaishi kimada, umetengana, au wewe ni mjane au mtalaka.)
  • usenge (kwa sababu wewe ni msenge au msagaji)
  • Mageuzi ya hali ya jinsia (kwa sababu unaishi au kutaka kuishi kama mtu mwenye jinsia kinyume na yako ya asili)
  • wajibu ya kuwatunza watoto au familia.

Bodi ya Kunzia Vitendo vya Ubaguzi pengine inaweza kukusaidia pia kama mtu fulani anatenda jinsi inavyofuata:
  • ambavyo hupendi.
  • ambavyo anakukasirisha, kukudhalilisha au kukutisha.
  • kwamba aidha ni kwa ajili ya jinsia, au kukuvisia kwa sababu zozote kama vile (kabila lako, jinsia yako na kadhalika) zinazoorodheshwa hapo juu.
Hii inaitwa unyanyasaji na ni kinyume cha sheria.

Piga simu kwa Bodi ya Kuzuia Vitendo vya Ubaguzi:
  • Sydney (02) 9268 5544
    Newcastle (02) 4926 4300
    Wollongong (02) 4224 9960
    toll free 1800 670 812
  • Tele-typewriter (TTY) kwa viziwi au watu ambao wana ulemavu wa kushikia (02) 9268 5522
  • Huduma za Utafsiri au Ukalimani kwa mkalimani wa simu 131 450
Au ongea na wafanyakazi wa mtaa wako wa jamii.




Previous Page | Back to Lawlink Home | Top of Page
  Last updated 15 November 2007   Crown Copyright ©  
Hosted by agd logo
Lawlink NSW